Kozi ya mchezo wa mpira wa wavu ya makocha iliyoandaliwa na shirikisho la mpira wa wavu huumu nchini ilikamilika leo katika ukumbi wa kilabu cha michezo cha ABSA jijini Nairobi. Kozi hiyo ya siku sita iliyoendeshwa na Geoffrey Onyango, Teresia Mudengani, Kevin Owuor na Richard Sylvain iliwashirikisha makocha 28 wa mchezo huo kutoka kote nchini.